27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

ZIDANE: SINA HOFU NA MACHAFUKO YA KATALUNYA

MADRID, Hispania

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane, amesema ataendelea kukiandaa kikosi chake katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ dhidi ya Girona licha ya kuwapo kwa hofu ya kuahirishwa kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyoko Jimbo la Katalunya, Hispania.

Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Estadi Montilivi, unaweza kuahirishwa kwa sababu za kisiasa zilizoathiri eneo hilo ambapo mamia ya wapiga kura walijeruhiwa na askari wakati wakijaribu kusimamisha zoezi la upigaji kura kudai uhuru na kujitawala.

Wananchi wa eneo hilo walipiga kura siku ambayo Barcelona walicheza na  Las Palmas. Mchezo ulichezwa bila mashabiki baada ya uwanja kufungwa lakini Zidane anadai kwamba ana matumaini na ulinzi utakuwapo katika uwanja huo ili kuhakikisha hakuna atakayejeruhiwa.

Zidane akizungumza hivi karibuni baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya  Fuenlabrada katika michuano ya Copa del Rey, alisema hana shaka ya usalama katika mchezo wao ujao.

“Hatuna shaka kuhusu Katalunya kwa sababu tuna imani ulinzi utaimarishwa, tutacheza mchezo wetu bila kufikiri jambo lolote baya kama linaweza kutokea, tunatarajia utakuwa mchezo mzuri.

“Tutajiandaa na mchezo wetu ujao jambo ambalo ni wajibu wetu kufanya hivyo, tunajaribu kuwa kawaida bila kufikiri jambo lolote baya kama linaweza kutokea,” alisema Zidane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles