30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

TAKUKURU WAPEWA NENO LA UJASIRI

Na PATRICIA KIMELEMETA -DAR ES SALAAM

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika, jana aliwataka watendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), wasiruhusu kuingiliwa na wanasiasa wanapotekeleza majukumu yao.

Akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuchika aliwataka wasikubali kutishwa na mtu yeyote kwa sababu kazi  wanayoifanya inaakisi utendaji  wao kisheria.

Waziri Mkuchika wakitekeleza hayo watajijengea ujasiri wa kutekeleza malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuanzisha Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

“Mnapaswa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha mnatenda haki kwa wananchi. Simamieni weledi, uadilifu na uwajibikaji ili muweze kuakisi kazi mnazofanya kisheria.

“Hakuna kumvumilia mtumishi anayekiuka maadili ya kazi yake ikiwa atabainika kuomba au kupokea rushwa anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola alimweleza Waziri Mkuchika kuwa taasisi yake imekuwa ikiingiliwa na baadhi ya wanasiasa inapokuwa ikitekeleza majukumu yake.

“Kuna baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitumia jina la Takukuru kwa ajili ya kujikuza kisiasa, jambo hili halikubaliki kwa sababu tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na wala hatutaki kuingiliwa,” alisema Mlowola.

“Ninakuomba Waziri, ulichukue hili na ukienda bungeni ukawaelimishe wabunge na wasiasa wengine ili wajue kazi zetu,” alisema Mlowola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles