33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

WIZARA YATOA MAGARI 12 KUENDELEZA SHUGHULI ZA UVUVI

Na JOHANES RESPICHIUS -DAR ES SALAAM

WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, imekabidhi magari 12 kwa wakurugenzi wakuu na viongozi wa taasisi na vitengo wa mradi wa kitaifa wa unaohusisha shughuli za maendeleo ya uvuvi,  Southwest Indian Ocean Fisheries Covernance and Shared Growth (SWIOFish).

Magari hayo ambayo yamefadhiliwa na Benki ya Dunia, yamegharimu Sh bilioni 1.4 na yalikabidhiwa na Katibu Mkuu wa Uvuvi, Dk Yohana Budeba, kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dk. Charles Tizeba.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Budeba alisema mradi huo unahusisha nchi zilizoko Magharibi mwa ukanda wa Bahari ya Hindi, ambapo kwa Tanzania ulianza Juni 22, 2015, ikiwa na lengo la kuzijengea uwezo wa nchi katika kusimamia rasilimali za bahari.

“Pamoja na mchango wa uvuvi kuwa mkubwa katika taifa, sekta hii imekuwa na changamoto nyingi, zikiwamo uvunaji usio endelevu kwa rasilimali  za uvuvi, hivyo kuhatarisha ajira za Watanzania.

“Changamoto nyingine ni kuwapo kwa uhaba wa taarifa za kitafiti na takwimu sahihi za uvuvi kuhusu vitendo haramu, upungufu wa elimu na uelewa kwa sehemu kubwa ya jamii kuhusu matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi,” alisema Dk. Budeba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles