32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

KAMPUNI YA BURUNDI YAAHIDI KUITUMIA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Minolacs ya Burundi, imeahidi kuendelea kuitumia Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kuridhika na ufanisi wa hali ya juu wa kuhudumia shehena ya ngano tani 12,000 za kampuni hiyo hivi karibuni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Munir Bashir, aliyasema hayo katika barua yake ya shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, ambapo pamoja na mambo mengine alielezea jinsi Bandari ya Dar es Salaam ilivyo na ufanisi bora.

“Tunashukuru sana menejimenti ya TPA na wafanyakazi kwa utendaji wenu mzuri na wa hali ya juu uliowezesha kuhudumia shehena yetu iliyoletwa na meli ya MV Loving.

“Tunawashukuru sana na tunaahidi kuongeza shehena kufikia tani 16,000 za ngano tutakazopitisha Bandari ya Dar es Salaam wiki ya kwanza ya Oktoba mwaka huu,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Minolacs ni kampuni binafsi inayojishughulisha na biashara ya nafaka, kwa ajili ya chakula yenye uwezo wa mauzo ya kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 6.8 kwa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles