32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

HATI YA MASHTAKA YAKWAMISHA KESI YA MMILIKI LUCKY VINCENT

Kesi ya makosa ya usalama barabarani ikiwamo kusafirisha watoto bila vibali inayomkabili mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent, Innocent Moshi, imekwama kusikilizwa leo baada ya Mahakama kuamuru upande wa Jamhuri kuifanyia marekebisho hati ya mashtaka.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Desderi Kamugisha ametoa amri hiyo leo baada ya Wakili wa utetezi Method Kimogoro, kuweka pingamizi kuhusu hati hiyo ya mashtaka.

Ushahidi wa kesi hiyo ulipangwa kuanza leo ambapo upande wa jamhuri ulitarajia kuwa na mashahidi watatu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 6, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya mashahidi watatu wa jamhuri kutaanza kutoa ushahidi wao.

Moshi na wenzake wanadaiwa kusafirisha wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent bila kuwa na vibali muhimu na kusababisha ajali ya wanafunzi 32 na walimu wawili wa shule hiyo na dereva mmoja, mjini Arusha Mei mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles