“Nataka watu wajue kwamba, LaMotta alikuwa bondia mwenye uwezo wa hali ya juu, wengi wataendelea kumkumbuka kutokana na nguvu zake, ucheshi, akili akiwa ulingoni, uchekeshaji pamoja na mambo mengine mengi,” alisema mke wa LaMotta.
LaMotta alizaliwa Julai 10, 1922, mjini New York, lakini wazazi wake walikuwa na asili ya nchini Italia, aliamua kuingia kwenye ngumi baada ya kukataliwa kujiunga na jeshi la Marekani kutokana na kuwa na matatizo ya kiafya.
Pambano lake la kwanza ambalo lilimpa umaarufu mkubwa duniani lilikuwa mwaka 1943, baada ya kumchapa mpinzani wake Sugar Ray, hivyo aliweza kujikusanyia idadi kubwa ya mashabiki kwa kuwa ulikuwa ni mwaka wake wa pili tangu atambulike kwenye chama cha ngumi nchini humo.
LaMotta katika maisha yake ya ngumi alifanikiwa kucheza jumla ya mapambano 106 na kufanikiwa kushinda 83, huku 30 akishinda kwa KO, wakati huo 19 akipoteza na manne akitoka sare.
Katika maisha yake ya ngumi aliwahi kuvunjika pua mara sita, mkono mara sita, kuvunjika mbavu pamoja na kupata tatizo la macho mara tano, lakini bado aliamini kuwa ngumi ni mchezo wa sehemu ya maisha yake.
Bondia huyo alitangaza kustaafu ngumi mwaka 1954, baada ya hapo akaamua kuingia kwenye filamu pamoja na uchekeshaji.