24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

UCHAGUZI WA MARUDIO KENYA SASA OKTOBA 26

NAIROBI, KENYA

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), imebadili tarehe za uchaguzi wa urais wa marudio uliotokana na uamuzi wa Mahakama ya Juu kufuta matokeo yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Agosti 8.

Awali ikiwa imepanga uchaguzi ufanyike Oktoba 17, wakati mahakama ilipotoa uamuzi wa kuufuta Septemba Mosi 2017, sasa imeusogeza hadi Oktoba 26.

Uamuzi huo umekuja baada ya Baraza la Mawaziri kupitisha bajeti ya Sh bilioni 10 za Kenya kwa uchaguzi huo na siku moja baada ya Mahakama ya Juu kutoa hukumu yake nzima kuhusu sababu za kufuta uchaguzi.

Uamuzi huo wa kufuta uchaguzi ulitarajiwa kutokana na mwelekeo wa mambo, ikiwamo mfumo wa kusambaza matokeo kuhitaji muda zaidi kuurekebisha kwa kuondoa takwimu zinazohusu uchaguzi wa Agosti 8.

Wakati huohuo, Rais Uhuru, jana aliendelea kuishambulia Mahakama ya Juu, akisema uamuzi wake wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti  8, ni mapinduzi yaliyofanywa na majaji wanne.

Alisema hukumu nzima ya ufutaji matokeo ambayo ilitolewa juzi ni  udikiteta wa kijaji, ambao umewapora Wakenya mamlaka ya kufanya uamuzi.

“Haya yalikuwa mapinduzi, lazima niseme hivyo,” alisema wakati akikutana na viongozi wa Chama cha Jubilee kutoka Kaskazini mwa Kenya, Ikulu jijini Nairobi jana.

“Hii ni sauti ya wachache, ambao wameamua kwamba wanaweza kuwachagulia wengi wa Wakenya kiongozi. Iwapo huu si udikteta, sijui ni nini tena,” alisema.

Alisema mafanikiio ya Katiba ya 2010 yamepinduliwa na hukumu, ambayo inaruhusu watu wachache kuongoza wengi.

“Hukumu imeonyesha kuwa sauti za watu hazina maana, bali sauti za wachache ndiyo muhimu, ambao wanajawa na kiburi cha kujipa madaraka ambayo hawana,” alisema.

Alisema hukumu ya Jaji David Maraga haiendani na maana iliyopo katika Katiba.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles