32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

BAVICHA WATAKA KUANDAMANA KULAANI KUSHAMBULIWA LISSU

 

Na ASHURA HUSSEIN


BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Mkoa wa Kagera limetangaza kuandaa maandamano ya amani kulaani tukio la kushambuliwa kwa risasi Mwanasheria Mkuu wa chama chao, Tundu  Lissu  Septemba 7, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Bavicha Manispaa ya Bukoba,  Ishengoma Audax alisema licha ya kuandamana watakwenda katika Hospitali ya Rufaa Bukoba kuchangia damu.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kagera, Francis Rutta alisema wameamua kuandamana kulaani kushambuliwa kwa Lissu na kuvitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinawakamata na kuwatia mbaroni wahusika.

“Tunafanya maandamano ya amani hivyo hatutegemei polisi kuzuia maandamano yetu kwa kuwa ni ya amani.

“Lakini tunaunga mkono uamuzi wa Brlaza Kuu la Taifa Bavicha linaloongozwa na Mwenyekiti Patrobas Katambi,” alisema.

Alisema wamekuwa wakishangazwa na hatua ya polisi kuwazuia wananchi kumuombea Tundu Lissu ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa makada wa chama chao waliovaa fulana zenye ujumbe wa kumuombea.

Alisema  huo ni ukiukaji mkubwa wa demokrasia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles