29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAASKOFU, WACHUNGAJI 700 KUOMBEA NCHI AMANI KESHO

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jaffo, kesho anatarajia kuungana na maaskofu na wachungaji mkoani Dodoma kufanya maombi ya pamoja kuombea amani ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Mkoa wa Dodoma, Askofu Dk. Damas Mukasa, alisema Jafo anatarajiwa kuongoza maombi hayo ya siku mbili.

Askofu Dk. Mukasa alisema kuwa pamoja na viongozi hao wa kanisa, pia maombi hayo watashiriki wafanyabiashara mbalimbali.

Alisema kuwa jumla ya maaskofu na wachungaji wapatao 700 kutoka makanisa mbalimbali watakutana kwa siku mbili kufanya maombi na kujifunza habari mbalimbali ambazo zitaimarisha amani ya nchi.

“Idadi hiyo ya watumishi kwa kushirikiana na naibu waziri huyo pamoja na wafanyabiashara, tutafanya maombi kwa ajili ya kuiombea nchi yetu amani iendelee,” alisema.

Akifafanua mwenyekiti huyo alisema kuwa pamoja na viongozi wa dini kushughulika na huduma za kiroho, pia wanatakiwa kupewa elimu ya uchumi ili waweze kujikimu katika maisha yao ambayo yatawawezesha kutatua changamoto kama vile kuwasomesha watoto, matibabu na kwenye kilimo.

Mwenyekiti huyo akielezea juu ya umoja huo, alisema kuwa lengo ni kuhakikisha makanisa yanaungana kwa pamoja katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ambazo zinagusa jamii na Serikali kwa ujumla badala ya kufanyika kwa kanisa moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles