24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

WAGOMBEA CCM ZANZIBAR KUJADILIWA KESHO

Chama Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar, kesho kinatarajia kuchuja majina ya wagombea walioomba ridhaa ya kugombea  nafasi ya uenyekiti wa wilaya kwa kipindi cha mwaka 2017-2022 visiwani humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalumu ya ya CCM Taifa (NEC), Waride Bakari Jabu,  pamoja na mambo mengine kitajadili hali ya kisiasa ya Zanzibar na taarifa mbalimbali kutoka katika idara na vitengo vya chama hicho.

“Vile vile, kikao kitapokea na kujadili majina ya wana-CCM waliojitokeza kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM ngazi ya wilaya na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa,” amesema Jabu katika taarifa yake hiyo.

Kikao cha kesho kitakachofanyika katika Ofisi Kuu za chama hicho, Kisiwandui Visiwani humo, kimetanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati ya NEC-Zanzibar kilichofanyika jana visiwani humo na kuongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk. Abdulla Juma Sadalla, kwa ajili ya kuandaa ajenda za kesho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles