31.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

WANANCHI WAIBA MAJI KUFYATULIA MATOFALI

Na Ahmed Makongo


 

BAADHI ya wananchi wa mitaa ya Nyasura na Bunda Stoo, katika Halmashauri ya Mji wa Bunda, wanadaiwa  kukata mabomba na kuiba maji kwa ajili ya kufyatulia matofali.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji katika Halmashauri ya Mji wa Bunda,   Jumanne Tubert alisema hali hiyo inasababisha wananchi wengine kukosa huduma hiyo na kusababisha hasara kwa serikali.

Alikuwa akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, wakati akikagua mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa wilayani hapa.

Tubert alisema wananchi hao wamekuwa wakiharibu miundombinu hiyo ya maji na kuiba maji kwa ajili ya kufyatulia matofali.

Alisema jambo hilo limekuwa likisababisha hasara kubwa kwa mamlaka hiyo huku baadhi ya wananchi waliounganishiwa huduma hiyo wakikosa maji kutokana na kupotea bure.

“Mkuu kupitia kwako naomba nifikishe ujumbe huu maana wananchi wa Nyasura  na Bunda Stoo kule chini wakati wa usiku wanakata mabomba na kuiba maji kwa ajili ya kufyatulia matofali.

“Tunakuoma utusaidie jambo hili   liweze kukomeshwa,” alisema Tubert.

Alisema  hali hiyo imekuwa ikisababisha upotevu mkubwa wa maji na kuisababishia hasara kubwa mamlaka hiyo.

Bupilipili  alishauri   watu hao wasakwe na kukamatwa mara moja ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Alisema serikali kamwe haiwezi kuvumilia hali hiyo ya kuhujumu miundombinu ya maji   wilayani hapa.

“Hao wanaoharibu miundombinu na kuiba maji muwakamate mara moja na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

“Serikali haiwezi kukubali kuona miundombinu ya maji inaharibiwa na watu wachache wasiotaka maendeleo,” alisema   Bupilipili.

DC aliiagiza mamlaka hiyo kuhakikisha wateja wote wa maji wanalipia bili zao benki na siyo kulipia dirishani kama ilivyo kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles