27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE AHOJI USUMBUFU KWA VIJANA WANAOUZA FEDHA TUNDUMA

NA RAMADHAN HASSAN

MBUNGE wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema), ameitaka serikali ieleze ni kwanini  imekuwa ikiwasumbua vijana ambao wanafanya biashara ya kuuza fedha na kudai kuwa, wafanyabiashara hao hawalipi kodi.

Mwakajoka, akiuliza swali la nyongeza jana bungeni, aliitaka serikali itoe tafsiri sahihi kwa vijana ambao wananunua fedha mipakani na kuziuza katika mabenki ya ndani kama ni miongoni mwa wafanyabiashara wanaolipa kodi au la.

“Kumekuwapo na tafsiri isiyo sahihi kwa vijana wanaonunua fedha kutoka nchini Zambia (Kwacha) katika Mji wa Tunduma kuwa hawalipi kodi ya serikali.

“Wakati wakinunua huenda nazo Lusaka, Zambia na kununua Dola za Marekani na kuja kuziuza katika benki  zetu, na ndipo serikali inapokusanya kodi, je, ni kwa nini serikali inawasumbua wakati kwanza wanaingiza fedha za kigeni nchini na huku ikijua kuwa hakuna benki yoyote inayonunua Kwacha ndani ya nchi. .

“Je, ni lini serikali itatambua mchango wa wananchi hawa badala ya kuwaona kama si walipa kodi,” alihoji Mwakajoka.

Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Same Magharibi, Mathayo David (CCM), alitaka kujua serikali ina mikakati gani ya kuongeza ukwasi katika mabenki na wananchi wa kawaida ili washirikiane na serikali katika kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja, kaya na taifa kwa ujumla.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, alisema vijana ambao wanafanya biashara hiyo wanaliingizia taifa pato, hivyo hakuna anayeweza kupinga kuwa hawalipi  kodi.

“Kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na Benki Kuu, hali ya ukwasi katika sekta ya fedha, hususan benki ni nzuri na hakuna vihatarishi vya kupelekea madhara hasi katika uchumi,” alisema Dk. Kijaji.

Alisema Benki Kuu itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha masoko ya fedha kwa lengo la kuhakikisha kwamba yanaendeshwa kwa ufanisi na ushindani na hivyo kusaidia kuongeza ukwasi miongoni mwa benki na taasisi nyingine za kifedha.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles