33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE ATAKA DORIA MAGENGE YA WAHUNI

NA RAMADHAN HASSAN

MBUNGE wa Viti Maalumu, Mariam Msabaha (Chadema), ameitaka serikali ieleze ina mkakati gani wa kufanya doria katika maeneo mbalimbali ili kubaini magenge ya wahuni.

Mbali na hilo, aliitaka serikali ieleze ina mikakati gani ya kuzuia uuzwaji wa silaha za jadi katika maeneo mbalimbali, kama vile minadani na maeneo ya wazi na kutaka kujua je, ufanyaji wa biashara hauwezi kuongeza vitendo vya kihalifu.

Akiuliza swali jana bungeni, Mbunge huyo alihoji serikali inafanya nini kupambana na magenge ya watu wahalifu ambao wameonekana kuwa tishio kwa jamii.

Awali katika swali la msingi, Mbunge huyo alihoji serikali inalichukuliaje suala la uuzwaji wa silaha kiholela, kama vile mapanga na visu katika barabara na sehemu kama vile Ubungo na kusababisha watu kuwa na hofu kwa raia wema.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni, alisema kumekuwapo uuzaji holela wa silaha za jadi katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni barabarani, katika makutano ya Barabara ya Mandela na Morogoro eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Alisema kupitia Jeshi la Polis, linatambua tatizo hilo na tayari hatua mbalimbali za kudhibiti hali hiyo zimechukuliwa, ikiwa ni pamoja na operesheni  za mara kwa mara za kuwakamata wauzaji wa silaha za jadi barabarani kama mapanga, mikuki, upinde na mishale.

“Elimu inaendelea kutolewa kwa wafanyabiashara wa bidhaa au silaha hizo kutowapatia wauzaji wasio na eneo maalumu la kufanyia biashara hiyo,” alisema.

Masauni alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine Serikalini linaandaa utaratibu maalumu wa uuzaji wa bidhaa za aina hiyo na kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya biashara hiyo na kuwashauri wananchi waipige vita na kuepuka kujihusisha nayo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles