NAIROBI, Kenya
RAIS Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto, hatimaye wamewasilisha mahakamani stakabadhi zao kuhusiana na kesi dhidi yao iliyofunguliwa na Muungano wa vyama vya upinzani NASA.
Uhuru na Ruto waliwasilisha stakabadhi hizo Alhamisi, Agosti 24, ikiwa imesalia saa nne pekee ifike tarehe ya mwisho waliyotakiwa wawasilishe stakabadhi hizo. Akithibitisha hayo kwenye mitandao ya kijamii, Uhuru alisema kuwa yuko tayari kwa kesi hiyo. Haya yanajiri baada ya muungano wa NASA kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 8, wakidai kuwa haukuwa wa haki na huru.
Tayari NASA iliwasilisha stakabadhi za ushahidi katika mahakama kuu dhidi ya Uhuru na sasa wanasubiri kesi kusikizwa. Tume ya uchaguzi ya IEBC ilifuata mkondo huo huo na kuwasilisha stakabadhi zake zenye kurasa 54,000 katika mahakama kuu.