23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

RONALDO AOMBA KUONGEZEWA MSHAHARA

MADRID, HISPANIA

BAADA ya mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa UEFA kwa msimu wa 2016/2017, mchezaji huyo ameitaka klabu yake kumwongezea mshahara.

Ronaldo tayari amepeleka maombi yake kwa mkurugenzi wa klabu hiyo huku akisema anastahili kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani kutokana na uwezo wake wa kusaidia timu pamoja na tuzo anazochukua.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Ureno, Ronaldo anataka mshahara wake kwa wiki ufikie pauni 700,000, zaidi ya Sh bilioni 1 na milioni 983 na kuwapita wapinzani wake Lionel Messi na mchezaji mpya wa PSG, Neymar aliyejiunga na kikosi hicho kwa uhamisho wa pauni milioni 198 na kuchukua pauni 500,000 kwa wiki, sawa na bilioni 1 na milioni 416.

Hata hivyo, Ronaldo ambaye anachukua kiasi cha pauni milioni 21 kwa mwaka baada ya kukatwa kodi, anadai kwa sasa anataka mshahara wa pauni milioni 37, ili awe mchezaji wa kwanza kulipwa fedha nyingi duniani.

Hata hivyo, nahodha wa klabu hiyo, Sergio Ramos, ameonekana kumpigia debe mchezaji huyo akisema kwamba anastahili kuwa mchezaji namba moja anayelipwa fedha nyingi kutokana na uwezo wake na mchango anaoutoa.

“Kama mchezaji anakuwa bora duniani basi anastahili kuwa na kiwango kikubwa cha mshahara, lakini kwa upande wa wachezaji hatuna tatizo na si jukumu letu kuzungumzia suala hilo, ila ninaamini ni kazi ya viongozi,” alisema Ramos.

Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, amedai kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo, ila kikubwa anachokiangalia ni mipango ya kumwongezea mchezaji huyo mkataba mpya Novemba mwaka huu utakaomfanya aendelee kuwa hapo hadi 2021.

“Ronaldo ni mchezaji mwenye kiwango cha hali ya juu, tunachoangalia kwa sasa ni kumwongezea mkataba mpya mwaka huu ili kumfanya aendelee kuwa na furaha, tunaamini bado ana mapenzi ya kweli na klabu hii na uwezo wake ni mkubwa, siwezi kuzungumzia mambo ambayo yapo kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Perez.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles