25.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

MAGARI 22 YAZUIWA KUENDELEA NA SAFARI

Na JUDITH NYANGE -MWANZA

KIKOSI cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza kimeyazuia magari 22 kuendelea na safari na kuyatoza faini 79 baada ya kukutwa na makosa mbalimbali ikiwamo uchakavu wa matairi.

Akizungumza juzi baada ya kukamilika kwa ukaguzi wa magari uliofanyika katika Kituo cha Mabasi cha Nyegezi na Buzuruga, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema magari hayo yalizuiliwa kuendelea na safari hadi pale wamiliki wake watakapoyatengeneza.

Alisema wamekuwa wakipokea malalamiko mara kwa mara kutoka kwa abiria wa mikoani na nchi jirani kuhusu mabasi kuharibika mwendo mchache baada ya kuanza safari na abiria kupoteza zaidi ya saa saba yakiwa yanafanyiwa marekebisho.

“Kituo cha Mabasi Nyegezi na Buzuruga, magari 79 yalikaguliwa, 22 tuliyazuia kuendelea na safari hadi pale yatakapofanyiwa marekebisho na 55 tuliyaruhusu kuendelea na safari baada ya kurekebisha kasoro zilizobainika ikiwemo uchakavu wa tairi, tumekusanya Sh milioni 2.4 kutokana na makosa mbalimbali  ya barabarani tuliyoyabaini,” alisema.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza, Robert Hussein, aliwataka madereva na wamiliki wa magari kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha ni mazima.

“Tutakamata magari yote mabovu, mtu anayeona gari lake ni bovu, aliondoe barabarani yabaki magari mazima, tukilikuta tutang’oa namba uende ukatengeneze ulilete likaguliwe tena, ndipo tukuruhusu kuendelea na safari,” alisema Hussein.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles