29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

BUHARI ASONONESHWA NA HARAKATI ZA KUJITENGA NIGERIA

ABUJA, NIGERIA

RAIS wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amezungumza katika televisheni jana ikiwa hotuba yake ya kwanza tangu arudi nyumbani kutoka Uingereza alikokuwa akitibiwa, akilaani harakati za kutaka kujitenga zilizojitokeza wakati akiwa hayupo.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 74 ambaye alikuwa akitibiwa ugonjwa ambao haukuwekwa wazi, alionekana mwembamba na alisoma hotuba yake taratibu.

Aliapa kuwa ataongoza maradufu mapambano dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram.

“Nilisononeshwa kuona baadhi ya kauli wakati sipo, hasa katika mitandao ya kijamii ambazo zilivuka mipaka kwa kuthubutu kuhoji swala la uwapo wetu kama taifa. Hatua hii imevuka mpaka mno.

“Maridhiano ya kitaifa ni jambo bora zaidi katika kuishi pamoja kuliko kutengana,” alisema Buhari, ambaye alirudi Nigeria Jumamosi baada ya siku zaidi ya 100 nje ya taifa hilo la magharibi mwa Afrika lenye watu milioni 190.

Nigeria inakabiliwa na vuguvugu kadhaa zinazotishia kujitenga, ikiwamo kikundi cha uzalendo wa Biafra kikiongozwa na Nnamdi Kanu – mkosoaji mkubwa wa Buhari kusini mashariki wa nchi kunakotawaliwa na kabila la Igbo.

Kundi hilo limekuwa likizidisha harakati za kudai uhuru katika wiki za karibuni, huku Kanu akionekana pichani katika vikao na kundi la vijana wapiganaji wa kiume.

Aidha kuna Arewa, kundi la vijana wa Kiislamu wenye msimamo mkali, kaskazini mwa nchi, ambalo lilitoa amri hadi kufikia Oktoba Mosi kwa watu wa jamii ya Igbo kuondoka eneo hilo.

Aidha Boko Haram wamekuwa wakiendesha vita ya umwagaji damu kaskazini mashariki mwa nchi tangu mwaka 2009, ambayo imegharimu maisha ya watu 20,000 na wengine milioni 2.6 kukimbia makazi wakitaka kuanzishwa kwa taifa la Kiislamu.

Buhari alisema magaidi na wahalifu sharti wakabiliwe na kuangamizwa ili Wanigeria waweze kuishi kwa amani na usalama.

Rais huyo wa Nigeria alisema vita dhidi ya magaidi na wahalifu hayatawalenga tu waasi wa Boko Haram ambao wameanzisha upya mashambulizi, bali wanaowateka watu nyara, mapigano kati ya wakulima na wafugaji na pia ghasia za kikabila zinazochewa na wanasiasa wachochezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles