22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

WATAALAMU WAONYA KUUNDWA KWA ROBOTI ZINAZOUA

GENEVA, USWISI

ZAIDI ya wataalamu 100 wa teknolojia ya roboti wameutaka Umoja wa Mataifa (UN) kuchukua hatua ili kuzuia kuundwa kwa roboti zinazoweza kuua.

Kwenye barua kwa Umoja wa Mataifa (UN), wataalamu wa masuala ya teknolojia akiwamo tajiri Elon Musk, wameonya kuwa hatua hiyo itasababisha kuwapo kwa vita vitakavyohusisha roboti.

Wataalamu hao 116 wametaka kuwekwa marufuku ya kutumia teknolojia hiyo kuunda roboti inayoweza kutumiwa kama silaha.

“Wakati zikiundwa zitawezesha vita kupiganwa kwa kiwango kingine cha juu na kwa haraka zaidi kuliko vile ambavyo binadamu hufanya.

“Hizi zitakuwa silaha za ugaidi, silaha ambazo magaidi watatumia dhidi wa watu wasio na hatia, na silaha ambazo zitadukuliwa kubadili malengo yaliyokusudiwa,” iliongeza barua hiyo.

Mwaka 2015 zaidi ya wataalamu 1,000 na watafiti pia waliandika barua wakionya kuruhusua kuundwa kwa silaha kama hizo.

Kati ya wale walioweka sahihi barua ya mwaka 2015, ni pamoja na mwanasayansi Stephen Hawking na mwanzilishi mwenza wa Kampuni ya Apple, Steve Wozniak na Musk.

Roboti za kuua ni silaha ambazo zinaweza kuchagua na kuvamia kitu ambacho zinakilenga bila ya kuelekezwa na binadamu.

Wale wanaopendelea roboti hizo, wanaamini kuwa sheria za sasa za vita zinatosha kutatua shida yoyote ambayo itaibuka ikiwa zitatumiwa.

Lakini wale wanaozipinga, wanasema  roboti hizo ni tisho kwa binadamu na teknolojia yoyote ya kuziwezesha kuua inastahili kupigwa marufuku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles