SIFA ZA TWIGA ZA KIPEKEE
- Ni mnyama mrefu kuliko wote waishio ardhini.
- Hupenda amani mno.
- Ni mnyama ambaye wanyama wenzake wanaokula majani hujisikia amani kukaa naye kwa kuwa huona hatari tangu ikiwa mbali, sasa usishangae wanyama kama pundamilia, swala wakijaa chini yake.
- Akikupiga teke na likakupata uwezekano wa kupona ni mdogo, hata wanyama wanaomuwinda huliepuka teke hilo, anapoinua mguu utaona hata simba akikimbia.
- Anatumia miguu ya mbele kama silaha yake wakati wa mapigano, nyuma hutumia inapibidi kama anapambana na mnyama zaidi ya mmoja ila ni nadra.
- Anahusudu kujitafuna, muda mwingi huutumia kwa kula
- Ni mnyama mtalii anayependa kushangaa ulimwengu ulivyo, ndio maana hutumia muda wake wa ziada katika kutembea.
- Wakati wanyama wengine wakitumia muda mwingi kulala, pengine twiga ndio kiumbe pekee ambaye hulala muda mfupi kuliko viumbe wengine wote, hutumia saa mbili hadi nne tu, kama ana mtoto ndio yatakuwa pungufu ya hapo katika saa 24.
- Kiumbe huyu ana moyo mkubwa pengine ndio sababu wanavumilia mengi, moyo hufika hadi kilo kumi.
- Shingo yake ndio sehemu inayomsisimua kimahaba, wanapokutana dume na jike hufanya mchezo kama wa kuzungusha kwa kuzifunga shingo zao, mchezo huo humfanya dume kumpanda jike wake.
- Twiga jike ni maminifu kwa dume lake, jike naye hutafuta dume jingine endapo dume wake atakamatwa na wanyama wala nyama au kufa kwa ugonjwa na kama atakosa anaweza kufa kwa upweke.
- Wakati jike akiwa na sifa hizo kwa dume ni tofauti kidogo, lenyewe hupendelea majike wanaochipukia na wakati mwingine huweza kumpanda jike mwingine hata mbele ya jike wake.
- Binadamu anaweza kupita katikati ya miguu ya twiga kijana bila kugusa mwili wake, na bado ikabakia nafasi kubwa juu.
- Wanyama wanaowinda kama mnyama wanayemtafuta yupo jirani na twiga, huamua kubadili windo kwa kuwa twiga huharibu mbinu zao kwa sababu huwaona kwa urahisi.
- Ni mnyama ambaye si mvivu na ana madaha pindi atembeapo.
Mnyama huyu pamoja kwamba ni mpenzi wa amani, lakini usije ukamsogelea maana akikuhisi vibaya anaweza kukujeruhi kwa kurusha miguu yake, hivyo ni jambo jema kama utakuwa unamtazama kwa mbali kidogo na ukawa mtulivu kama alivyo yeye.