22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

UTAFITI: WANAFUNZI WA PHD WANAONGOZA KUUGUA AFYA YA AKILI

Na Joseph Lino

Wanafunzi wanaosoma taaluma mbalimbali katika ngazi ya PhD huwa na muda mwingi katika masomo, ambao huutumia kufanya tafiti za masomo ili kuthibitisha kama unastahili kutunikiwa Shahada ya udaktari (PhD).

Wanafunzi wa PhD hukumbwa na vikwazo mbalimbali katika kipindi cha masomo kama msongo wa mawazo kutokana kutochapishwa kwa tafiti zao, pia tabia ya unyanyasaji au ukosefu wasimamizi ambao hawana uzoefu wa kutosha.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la Research Policy nchini Uingereza mwaka huu, unasema kuwa msongo wa mawazo unaweza kuwa na athari kwa akili ya wanafunzi wa PhD.

Takribani theluthi moja ya wanafunzi wanaosoma PhD wapo katika hatari ya kupata matatizo ya akili.

Uchunguzi ulifanywa kwa wanafunzi 3,659 kutoka vyuo vikuu huko Flanders, Ubelgiji, kwa wanafunzi wa masomo ya Sayansi au Humanities.

Hata hivyo, matokeo ya uchunguzi huo yalionesha jinsi taaluma inavyoathiri afya ya akili.

Asilimia 51 ya watu waliofanyiwa utafiti walingundulika kuwa na dalili aina mbili za matatizo ya akili, huku asilimia 32 waliripotiwa kuwa na dalili aina nne.

Kiwango hicho kilikuwa  cha juu mara mbili zaidi ya idadi ya watu wenye elimu ya juu.

 

Baadhi ya dalili za kawaida ambazo wanafunzi waliripoti kuwa nazo ni pamoja kupoteza usingizi kutokana na hofu au wasiwasi na kutoweza kufurahia shughuli zao za kila siku.

Watafiti pia waligundua kuwa jambo kubwa linalosababisha matatizo ya akili ilikuwa ni kushindwa kutimiza mahitaji ya familia kutokana na kazi nyingi.

Uhitaji mkubwa wa masomo ya PhD na kushindwa kudhibiti kazi wanazopewa.

 

Mwanafunzi wa PhD kutoka chuo cha Imperial nchini Uingereza, Claire anasema kusoma katika ngazi ya Uzamivu kuna uwezekano wa kuathiri afya ya akili ya mtu.

Anasema baadhi ya marafiki zake walifikiria kuacha kuendelea na chuo katikati ya masomo yao.

Claire anaelezea kuwa alianza kusikia maumivu ya mwili, mafua makali  na homa. Hata hivyo, vipimo vya damu vilionesha kuwa hakuna tatizo lolote, ingawa madaktari walimwambia hali kama hiyo inawezekana  inahusiana na msongo wa mawazo.

Hata hivyo, anasema kuwa  si kila mtu anayesomea PhD  anaelewana na msimamizi wake, ukweli ni kwamba, baadhi ya wasimamizi hawana msaada na manufaa, bali hudharau wanafunzi.

Ripoti ya Research Policy inasema mfumo wa wasimamizi kwa wanafunzi wa PhD  ulionekana ni jambo linalochangia matatizo ya akili kwa wanafunzi.

 

Research Policy wanapendekeza kuwa vyuo vikuu viongeze juhudi zao katika  kufuatilia wanafunzi wenye matatizo akili na kuongeza mbinu za usimamizi na kutambua kwa ujumla hatari na sababu za msingi.

Naye Nathan Vanderford, mwalimu msaidizi katika Chuo Kikuu cha Kentucky nchini Uingereza, ambaye pia ni mtalaamu wa afya ya akili kwa wasomi, anasema tafiti hiyo inaonesha namna mazingira ya kazi kwenye taaluma inavyochangia utulivu au matatizo ya akili kwa wanafunzi wa PhD.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles