28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE CHADEMA KUWASILISHA HOJA BINAFSI UKATILI WA JINSIA

 

Na NORA DAMIAN -DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest (Chadema), amesema anatarajia kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhakikisha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinatokomezwa.

Amesema licha ya kuwapo kwa sheria kali dhidi ya watu wanaofanya vitendo hivyo, bado matukio hayo yameendelea kuripotiwa kila kukicha huku waathirika wakubwa wakiwa ni watoto.

Akizungumza Dar es Salaam jana, alisema amefikia hatua hiyo kutokana na kuendelea kuwapo vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto wa kike hasa Dar es Salaam huku wengi wao wakiwa ni wanafunzi.

“Takwimu za Idara ya Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala zilizowasilishwa katika Baraza la Madiwani wiki iliyopita zinaonyesha katika robo ya tatu ya mwaka, zaidi ya watoto 200 wamefanyiwa ukatili wa aina mbalimbali, hali hii inasikitisha sana.

“Nimewasiliana na wanasheria kadhaa waniandalie mapendekezo ambayo nitayapeleka bungeni wote waliopata madhila haya wapate nafasi ya pili ya elimu,” alisema Anatropia.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, kati ya watoto hao 85 wamebakwa, 20 wamelawitiwa, saba wamepigwa vibaya, 74 wametelekezwa, 51 wamenyanyaswa kijinsia na 17 wamebakwa na kulawitiwa.

Alisema hilo ni ongezeko la matukio 137 ikilinganishwa na 107 ya mwaka jana.

“Kama katika halmashauri moja hali iko hivi je, vipi katika halmashauri zingine. Tunaweza tukahukumiwa kama wazazi, kama taifa ama kama wabunge, nataka umma wa Watanzania unisikie utoke ndotoni na kwa pamoja tusaidiane kuokoa kizazi hiki,” alisema.

Pia aliiasa jamii ijihadhari na kuruhusu utani usiofaa unaofanywa na watu wazima dhidi ya watoto kama vile kumuita mtoto mchumba kwa sababu  umekuwa ukijenga uhusiano hasi kwa watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles