22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

LUKUVI AZINDUA MRADI WA SAFARI CITY ARUSHA

Na Hassan Mabuye -Arusha

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amezindua ujenzi wa Mji wa Safari pamoja na kuwapa hati  wakazi 100 wa mji wa Arusha.

Safari City ni mji wa kisasa uliopangwa vizuri kwa kufuata sheria na kanuni za mipango miji na eneo hilo limepangwa viwanja vya nyumba za makazi, ofisi, biashara, hoteli, shule na viwanda vidogo vidogo.

Viwanja hivyo vina huduma zote muhimu kama vile miundombinu ya maji, umeme, barabara na mfumo wa majitaka.

Mauzo ya viwanja hivi yanakwenda sambamba na mauzo ya nyumba za mfano ambako viwanja vya makazi vinaanzia Sh milioni saba na kuendelea.

Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi alipokea taarifa ya kufutwa mashamba 12 yaliyoko Halmashauri ya Meru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,208FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles