25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA UDSM AWA MTAWA, AGAWA MALI ZOTE

Na MWANDISHI WETU,

PROFESA mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Josephat Maghway (65) jana aliamua kufunga nadhiri za daima za maisha ya utawa katika Kanisa Katoliki la Salvatorian la Chuo Kikuu cha Jordan mkoani Morogoro.

Taarifa ambazo gazeti hili lilizipata jana kupitia marafiki wa karibu wa Profesa huyo, zilieleza kuwa,  kabla ya kuingia utawa na kufunga nadhiri hizo, aligawa vitu vyote ikiwamo nyumba, magari na mashamba kwa taasisi za dini.

“Leo (jana) ndio amefunga nadhiri za daima za maisha ya utawa ambapo amekula kiapo cha kuishi maisha ya kujitolea kwa ajili ya watu maskini kwa kuuza kila alicho nacho na kuwagawia maskini na yeye kuamua kuishi maisha ya nadhiri ya ufukara, utii, na usafi wa moyo,” alisema Faraja Chrysostom ambaye ni rafiki wa karibu.

Alisema ingawa Profesa Maghway anapenda kuishi kitawa lakini shirika lake likitaka linaweza kumpatia upadri.

Akielezea tukio hilo la kuweka nadhiri, alisema Profesa huyo aliungana na watawa wengine wanne wa shirika  la Mtakatifu Francis wa Assizi wa Kapuchini walioko Kola, Morogoro kufanya agano hilo.

Profesa Maghway alistaafu kufanya kazi UDSM akiwa na miaka 60 mwaka 2010 na inaelezwa  hakuwahi kuoa wala hana watoto.

Profesa Maghway alipongezwa na watu mbalimbali wakiwamo marafiki zake ambao waliandika katika mtandao wa Whatsapp.

Miongoni  mwa waliompongeza ni Dk. Vincensia Shule wa kitengo cha Sanaa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye aliandika katika kundi moja la mtandao wa Whatsapp kuwa;

“Kwa namna ya kipekee kabisa napenda kumpongeza Prof. Josephat Baran Maghway kwa kuweka nadhiri ya kudumu ya Utawa…amefanya mengi kwenye taaluma akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Department of Foreign Languages & Linguistics (kitengo cha lugha) sasa ameamua kuendelea kumtumikia Mungu kwa next level (hatua nyingine mbele), Inshallah atakamilisha safari ya upadre”.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles