NA JESSCA NANGAWE
STAA wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amesema lugha ya Kiingereza ni muhimu zaidi kutumika katika filamu za kibongo, kwa kuwa wanatamani kufika mbali zaidi kimataifa.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliowakutanisha na Waziri wa Habari, Lulu alisema kutumia maneno ya Kiingereza ‘subtitle’ kwenye filamu zao ni muhimu, kwa kuwa ndiyo lugha inayowasapoti kuweza kufika mbali zaidi katika soko la filamu nje ya Tanzania.
“Hata uwakilishi wangu kimataifa ni kwa kuwa tuna subtitle kwenye kazi zetu na ndizo zinazotufikisha mbali zaidi, mi nadhani tuna kila sababu ya kuendelea kutumia lugha hiyo, wakati huo tukiendelea kuiwakilisha lugha yetu ya Kiswahili,” alisema Lulu.
Lulu aliongeza kuwa, wasanii wanapaswa kuwa na upendo, kwa kuwa ndio utakaowasaidia kuwa pamoja na kufanya wafike mbali zaidi katika kazi zao na kuachana na majungu.