32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUBORESHA CHUO CHA NIT

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

SERIKALI inakusudia kukiboresha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ili kiweze kwenda na teknolojia ya sasa na kuzalisha wataalamu watakaoweza kushindana katika soko la ajira la kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Prof. Zacharia Mganilwa, alisema chuo kimeanza kuboresha mindombinu kwa maana ya vyumba vya madarasa, ofisi za walimu pamoja na vifaa vya kufundishia kutokana na fedha zaidi ya Sh bilioni 6.5 zilizotengwa na Serikali.

Prof. Mganilwa, alisema kwa sehemu kubwa vyumba vya madarasa vimeboreshwa na kwamba chuo kinakusudia kuweka mkazo kwenye vifaa vya kufundishia katika sekta za anga na reli ili kwenda na wakati.

“Tangu kuanzishwa kwa chuo Serikali haijawahi kutenga fedha nyingi kama zilizotengwa mwaka huu, fedha hizo zitakiboresha chuo kwa kutoa wataalamu wa kisasa wakiwemo wa mambo ya usafiri wa reli, tutahama kutoka teknolojia ya treni za zamani na kuwa na wataalamu wa reli ya kisasa ambayo Serikali imeanza kujenga ya kiwango cha kimataifa,” alisema Prof. Mganilwa.

Alisema chuo hicho ni cha kipekee kinachotoa wataalamu wa aina yake katika ukanda huu wa Afrika na kwamba kinadahili wanafunzi waliofaulu katika kidato cha nne kwa masomo ya cheti na stashahada na wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kwa masomo ya shahada

Aliongeza kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda, wataalamu kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji ni muhimu ili kuratibu usafirishaji wenye tija na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji zisizokuwa za lazima zinazotokana na kutokusimamia vizuri usafirishaji wa malighafi na bidhaa zilizo tayari kwenda sokoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles