25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

WAOMBA KUVUNJWA BUNGE LA KATIBA

CARACAS, VENEZUELA

OFISI ya Mashitaka imeomba kuvunjwa kwa Bunge la Katiba ambalo lilitazamiwa kuapishwa jana nchini humo.

Ombi hili linafuatia uamuzi wa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Jamhuri, Luisa Ortega Díaz, ambaye aliomba kuanzishwa uchunguzi wa uchaguzi kuhusu Bunge la Katiba, ambapo upinzani ulitaja uchaguzi huo uligubikwa na wizi wa kura.

Wakurugenzi wanne wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wanalengwa na uchunguzi huo. Wanatuhumiwa kula njama na Rais Nicolas Maduro kuiba kura katika uchaguzi utakaofanyika kesho na kutangaza kiwango kikubwa cha ushiriki, ikilinganishwa na idadi halisi ya wapiga kura.

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Jamhuri, Luisa Ortega, ambaye ni kinara wa maandamano dhidi ya Rais Maduro, anataka uchunguzi kwa uchaguzi huo, pamoja na ushiriki wa wataalamu wa kimataifa. Kwa kusubiri hilo, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Jamhuri ameomba rasmi kuvunjwa kwa Bunge la Katiba.

Wakati huo huo, Rais Nicolas Maduro amesisitiza kuwa, Bunge la Katiba lilipaswa kuapishwa jana kama alivyotangaza.

Hata hivyo, jitihada za Ofisi ya Mashitaka zina uwezekano mdogo wa kufanikiwa. Jitihada zake za awali zilifutwa na Mahakama Kuu, inayoshutumiwa na upinzani kuegemea utawala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles