27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI KUZIWEKEA VIKWAZO URUSI

WASHINGTON, MAREKANI


BARAZA la Wawakilishi la Marekani limepiga kura kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini.

Urusi inaadhibiwa kutokana na kudaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka juzi, huku Korea Kaskazini na Iran zikiadhibiwa kwa majaribio ya nyuklia.

Muswada huo unatarajiwa kupitia Baraza la Seneti kabla ya kupelekwa kwa Rais Donald Trump ili auidhinishe na kuwa sheria kamili.

Akizungumza katika baraza hilo, David Ciciline kutoka Chama cha Democratic, alisema hatua kamili zinahitajika kuiwajibisha Urusi.

Alisema hawawezi kuruhusu dola nyingine kuingilia uchaguzi wao japokuwa rais wao anapinga kuihusisha Urusi na uchaguzi uliopita.

Naye Ted Poe kutoka Chama cha Republican, alisisitiza kuwa muswada unaihusisha Korea Kaskazini pia.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge la Urusi, Leonid Slutsky, alisema hatua hizo mpya zitazorotesha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles