29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI WENGI HUANZA ULEVI WAKIWA MATAIFA YA WATU

Na Joseph Lino,

KUSOMA chuo kikuu ni kipindi ambacho mwanafunzi huanza kujiendeleza, kujitengemea, kujitambua na kugundua mambo mbalimbali ya maisha.

Lakini mara nyingi mwanafunzi anapofika chuo kikuu huwa ndio mwanzo wa yeye kuanza kufanya starehe na mambo mengine mengi.

Starehe chuoni uhusisha utumiaji wa pombe na dawa ya kulevya.

Wanafunzi wengi huwa wanatumia kilevi kama kiburudisho, starehe na kutuliza akili huku wakifurahia kuperuzi  kwenye mitandao na marafiki.

Hata hivyo, utumiaji wa kilevi aina yoyote kunaweza kusababisha kuwa na tabia ya ulevi kwa mwanafunzi.

Kwa upande wa wanafunzi wa kimataifa ambao wanapata nafasi ya kwenda kusoma nchi za nje hasa mabara mengine huwa wanapatwa na changamoto za ulevi au utumiaji wa dawa za kulevya hivyo kusababisha kurudishwa nyumbani au kufeli masomo.

Wanafunzi wa kimataifa wakiwa masomoni huwa wanajifunza mambo mengi ikiwamo desturi na tamaduni za mataifa mbalimbali.

Hali hiyo, hufurahisha baadhi ya wanafunzi lakini wengine hujiingiza katika unywaji wa pombe kupita kiasi au dawa za kulevya na hivyo kushindwa kujikita kwenye masuala muhimu yatakayowasaidia hapo baadaye katika maisha yao.

Wengi wao kabla hawajajiunga na vyuo huwa na tabia njema lakini wanapofika kwenye mataifa ya watu huanza kufanya starehe zisizo na maana.

Utafiti uliyofanywa na Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani, umegundua kuwa wanafunzi wa kimataifa ambao wamekaa muda wa miezi mitatu hadi mitano huwa wanatumia kilevi kwa wastani wa asilimia nane kwa wiki.

Utafiti huo ulibanisha kuwa kati ya wanafunzi wa kimataifa 1,000 ambao walisoma nje takribani nusu walitumia kiasi kikubwa cha ulevi kuliko walipokuwa katika nchi anayotoka.

Asilimia 11 walibanika kuwa kwenye ulevi wa kupindukia wakiwa masomoni, wakati asilimia 29 walitumia dawa za kulevya ambapo asilimia 11 walijaribu kutumia dawa hizo kwa mara ya kwanza.

Kwa mujibu wa utafiti huo, wanafunzi waliokwenda kusoma Bara la Ulaya, New Zealand na Australia waligundulika kutumia kiwango kikubwa cha pombe.

Wanafunzi ambao walisafiri kwenda katika nchi ambazo unywaji wa pombe ni wa kiwango cha chini walikuwa na kiwango kidogo cha kilevi.

Wanafunzi waliokuwa na umri chini ya miaka 21 walitumia kiwango kidogo cha ulevi kabla hawajaenda kusoma nchi zingine.

Hata hivyo, baada ya kusafiri nje kiwango cha utumiaji wa pombe kiliongezeka hadi kufikia asilimia 170.

Baada ya kurudi nchini  kwao waliendelea kutumia pombe kwa kiwango kikubwa bila kujali mazingira.

Kwa upande wa wanafunzi waliokuwa katika nchi ambazo sheria hairuhusu mtu mwenye umri wa miaka 21 kunywa pombe, walikuwa wanajificha na kutumia kiwango cha juu cha ulevi.

Aidha, mambo mengine yanayochochea utumiaji wa pombe ilitajwa kuwa ni tamaduni na mazingira.

Katika nchi za Ulaya, vyakula vingi huwa vinambatana na mvinyo au pombe ambapo kutumia glasi moja kwa kila mlo kunaweza kusababisha ushawishi mkubwa wa ulevi.

Kitendo cha wanafunzi kuwa mbali na nyumbani katika nchi ya kigeni kunawatengenezea mazingira ya kutaka kuwa huru kwenye kujihusisha na starehe ya unywaji wa pombe kupita kiasi.

Wakati huo huo, wananfunzi wanaojihusisha na tabia ya ulevi katika nchi ya kigeni inaweza kuwaweka sehemu yenye hatari kubwa.

Mwanafunzi kuwa katika mazingira ambayo hayajui vizuri kunaweza kumuweka katika hatari kubwa ya matatizo au kuvunja sheria za nchi hiyo pamoja na kukamatwa au kurudishwa nyumbani.

Taasisi ya Forum on Education Abroad walibainisha kuwa kesi za wanafunzi wa kimataifa zinazoripotiwa zinahusiana na wizi, ujambazi na mauaji.

Hata hivyo, kwa upande mwingine, masomo yanayofundisha katika vyuo vya nje huwa na manufaa ya kuwawawezesha wanafunzi kujifunza namna ya kuwa bora na kuzoea mazingira.

Hata hivyo, wanafunzi wengi wanaosomo katika vyuo vya nje huwa na fursa kubwa ya kuajiriwa mara mbili na kupokea mshahara mkubwa tofauti na wanasoma nyumbani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles