Shirika la afya Duniani, WHO, limetoa tahadhari kuwa, ugonjwa wa zinaa wa kisonono, umeanza kuwa sugu dhidi ya dawa ya kupambana na ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika mataifa 77 tofauti Duniani, WHO imebaini kuwa maambukizi ya ugonjwa huo nchini Japan, Ufaransa na Uhispania, hayatibiki kabisa.
Lakini hata hivyo, shirika hilo linasema wengi wanaoambukizwa ugonjwa huo wako katika nchi masikini, ambazo zinavifaa duni kudhibiti ugonjwa huo.
Shirika hilo la Afya duniani linasema kufanya mapenzi bila ya kuingiliana na watu wachache wanaotumia kondomu kunasaidia kuenea kwa ugonjwa huo wa Kisonono