26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

VIONGOZI CHADEMA IGUNGA JELA KWA MKUSANYIKO USIO HALALI

Na ABDALLAH AMIRI

MAHAKAMA ya Wilaya ya Igunga  imewahukumu viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutumikia   kifungo cha mwaka mmoja jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko usio halali.

Waliohukumiwa kwenda jela ni aliyekuwa Diwani wa Kata ya Igunga ambaye kwa sasa ni Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Igunga,  Vicent Kamanga (52),  Mwenyekiti wa Chadema Tawi la Mwamsunga,  Fea Rifa (41) na Katibu wa Chadema Tawi la Mwamsunga katika Kijiji cha Mgongoro,  Luhanya Zogoma(48).

Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Igunga,  Elimajid Kweyamba, alidai  mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya,  Ajali Milanzi kuwa watuhumiwa wote watatu wakiwa wafuasi na viongozi wa Chadema  na wakiwa na nia ovu walifanya mkusanyiko usio halali wa Oktoba 30, 2016 kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni katika Kitongoji cha Mwamsunga wilayani humo.

“ Washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume na kifungu 74 na 75 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo,” alidai Kweyamba.

Watuhumiwa  walikana kutenda kosa hilo na  upande wa mashitaka uliwasilisha  mashahidi watatu mahakamani ambao   waliwatambua washitakiwa.

Akito hukumu hiyo, Hakimu Milanzi, alisema ushahidi uliotolewa    na upande wa mashitaka umewatia hatiani washitakiwa hivyo kila mmoja atatakiwa kutumikia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela.

“Mahakama inamwachia huru mshitakiwa wa nne ambaye alikuwa ni  Katibu wa zamani Chadema Wilaya ya Igunga, Idd Athumani, baada ya kukosekana  kwa ushahidi wa kumtia hatiani,” alisema Hakimu Milanzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles