24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MGEJA AMPIGA KOMBORA SPIKA WA BUNGE

Na HASTIN LIUMBA-DODOMA

MWENYEKITI wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation inayoshughulikia utawala bora na haki za binadamu, Khamis Mgeja, amemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai, kusimamia haki na usawa ndani ya Bunge.

Mgeja aliyasema hayo jana mjini hapa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

“Kwa sasa huko bungeni haki na usawa vinaonekana kutetereka kwa sababu tunaona wabunge wa upinzani wakifukuzwa bila sababu za msingi.

“Kutokana na kinachoendelea bungeni, baadhi ya Watanzania wameshindwa kumuelewa Spika Ndugai juu ya anavyoliendesha Bunge, kwani hata kauli zake hazifanani na cheo alichonacho.

“Yaani amefika mahali anakosa uvumilivu wa kuliongoza Bunge na nimefika mahali nashindwa kuelewa kama huyu Spika ndiyo yule ninayemfahamu au ni mwingine.

“Yaani amekuwa ni mtu wa kutoa kauli za kibabe, kauli za dharau na zinazoonyesha amekosa uvumilivu kwa wabunge wa upinzani.

“Kwa mfano, hivi juzi alipokuwa akiongoza Bunge, alitoa kauli na maneno ya kejeli juu ya wabunge wa upinzani waliofungua kesi mahakamani dhidi yake,” alisema Mgeja, ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

“Kwa hiyo, namshauri akajifunze kwenye mabunge mengine duniani ili akajue jinsi wanavyoendesha mabunge tofauti na yeye,” alisema.

Kwa mujibu wa Mgeja, kitendo cha Spika huyo kuendesha Bunge kwa kuwakandamiza wapinzani hakiwezi kuvumilika, kwa kuwa wabunge hao waliingia bungeni kwa mujibu wa Katiba.

Pamoja na hayo, Mgeja alimtaka Spika Ndugai awaombe radhi Watanzania kutokana na uwepo wa sheria mbovu za sekta ya madini zilizopitishwa na Bunge na yeye akiwa mmoja wa wabunge hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles