30.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

SAIDA KAROLI: NIMEKAA ‘JELA’ MIAKA 15

Na GLORY MLAY


WANAMUZIKI wa nyimbo za asili, Saida Karoli, amedai kwamba alikuwa jela ya muziki kwa miaka 15 iliyosababishwa na mikataba mibovu aliyowahi kuingia awali.

Saida Karoli alipotembelea Kampuni ya New Habari (2006) Ltd inayochapisha magazeti ya MTANZANIA, BINGWA, DIMBA na RAI wiki iliyopita, alisema sasa anajiona yupo huru kwa kuwa anaweza kuzungumza na waandishi wa habari na kufanya anachotaka kwenye muziki wake, kiasi kwamba anajiona yupo huru baada ya kuishi kwenye mikataba mibovu kwa miaka 15 tangu alipoanza muziki wake.

“Ile mikataba ilikuwa ya ajabu maana niliingizwa kwenye mikataba iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili cha ndani ambapo mimi sikuwa nikijua kusoma wala kuandika, pia nilikosa uhuru wa mawazo yangu na mambo mengine mengi ambayo kwa sasa nina uhuru ndiyo maana kuelekea miaka 15 tangu kuanza kwangu muziki najiona kama nilikuwa jela kwa miaka yote hiyo 15,” alisema Saida Karoli.

Saida Karoli kwa sasa anatamba na wimbo wa ‘Orugamba’ uliopo katika albamu yake ya nyimbo 17 na pia ameweka wazi kwamba hivi karibuni ataachia wimbo mwingine aliorekodi na Abelenego Damiani (Belle 9).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles