LOWASSA AITWA POLISI DAR

0
481

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ameitwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano leo.

Taarifa zilizopataikana jana kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, zilisema wito huo ulitolewa   na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Alimtaka Lowassa kufika Makao Makuu ya Polisi leo saa 4.00 asubuhi kwa   mahojiano.

Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alikuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia chama hichokwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.

“Taarifa ya Makene ilisema, ”Lowassa hajapewa maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo yatahusu nini hasa.

“Tayari chama kimetoa maelekezo kwa Kurugenzi ya Katiba na Sheria kuhakikisha   Lowassa anapata msaada wa sheria wakati wa mahojiano hayo.

“Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mahojiano hayo yanaweza kuhusishwa na kauli za Lowassa alizotoa   nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari   na Watanzania wengine wa dini ya Kiislamu waliokuwa katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan”.

Juzi akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, Lowassa pamoja na mambo mengine, alimtaka Rais Dk. John Magufuli kutafakari upya hatima ya masheikh wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumuki) maarufu ‘Uamsho’ wanaendelea kusota gerezani kwa miaka minne sasa bila kesi yao kusikilizwa, wakituhumiwa kwa ugaidi.

Alisema ni jambo la fedheha kwa nchi iliyopata uhuru zaidi ya miaka 50 kuwaweka mahabusu viongozi wa dini bila kesi kusikilizwa mahakamani.

Mara kwa mara Lowassa amekuwa akiitaka Serikali kuzingatia misingi ya utawala bora kama mojawapo ya misingi muhimu ya kuendesha nchi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Watanzania wote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here