Na ESTHER GEORGE
BAADA ya kuonekana amepungua katika picha mbalimbali za mitandaoni na kuzua minong’ono kwa baadhi ya mashabiki wake, Gift Stanford (Gig Money) amefunguka na kusema kuwa mpenzi wake, Mo J, ndiye anayetaka apungue.
Gigy ameongeza kwamba, mwonekano huo ndio unaoendana na umri wake, kwa kuwa bado msichana mdogo kiumri, hivyo mwili mkubwa kwake haumuonyeshi uhalisia wake.
“Mimi ni msichana mdogo, hivyo kuwa na mwili mkubwa siyo poa, lakini pia namridhisha mpenzi wangu Mo J, anapenda nikiwa hivi, anasema ndiyo navutia zaidi,” alisema Gigy, msichana asiyeishiwa vituko.
Hata hivyo, Gigy alisema wanaomfikiria vibaya kwamba anaumwa watakuwa wanakosea, amejipunguza unene kutokana na matakwa ya mpenzi wake anayempenda na hataki kupingana naye katika hilo.