33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

UINGEREZA YAONYA NJAMA ZA KUMPINDUA BUHARI

ABUJA, NIGERIA


SERIKALI ya Uingereza imeionya Nigeria juu ya kufanya mabadiliko ya Serikali yasiyo ya kidemokrasia.

Onyo hilo limekuja kufuatia minong’ono kuhusu mapinduzi ya kijeshi yanayochagizwa na wasiwasi wa afya ya Rais Muhammadu Buhari.

“Serikali ya Uingereza inaamini kwamba demokrasia ni muhimu nchini Nigeria. Kuna uchaguzi. Iwapo hufurahishwi na kiongozi wako, unatakiwa ubadili uongozi kupitia mchakato wa kidemokrasia na kupitia uchaguzi,” alisema Balozi wa Uingereza nchini Nigeria, Paul Arkwright wiki iliyopita.

Balozi Arkwright, alisema msimamo wa Uingereza uko wazi na unafahamika, na kwamba itatambua mabadiliko ya madaraka kupitia sanduku la kura pekee na si vinginevyo.

Alisema hayo pembezoni mwa tukio la uzinduzi wa ripoti mpya kuhusu rushwa nchini Nigeria, ambayo iliandaliwa kwa ushirikiano na taasisi ya sera ya Uingereza, Chatham House.

Kauli hiyo ilikuja siku moja baada ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nigeria, Tukur Buratai, kuonya kuwapo kwa nyendo zinazotia shaka jeshini za uwezekano wa mapinduzi kutokana na kuwapo ushirikiano baina ya maofisa wa jeshi na wanasiasa wanaoonekana kufanya vikao vya siri.

Rais Buhari alisafiri kwenda London, Uingereza wiki mbili zilizopita kwa matibabu ya ugonjwa ambao haukuwekwa wazi, ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kurudi nyumbani kutoka likizo ndefu ya afya yake.

“Ofisa yeyote wa jeshi au askari wa Nigeria atakayekutwa akijichanganya na watu wa aina hiyo au kujihusisha isivyo halali kisiasa, litakalomtokea tusilaumiane,” lilionya jeshi katika taarifa iliyosainiwa na msemaji wake, Brigedia Jenerali Sani Usman.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles