NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
DAWA ya meno ya Whitedent imepata tuzo ya kimataifa ya ubora inayojulikana kam SuperBrand, huku nafasi ya pili ikishilikiwa na Foma Gold.
Tuzo hiyo imetolewa baada ya utafiti uliofanywa na Kampuni ya Kimataifa ya utafiti wa ubora wa bidhaa ya nchini Uingereza inayojulikana kama The Centre for Brand Analysis.
Katika utafiti huo uliofanyika katika masoko kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza kwa kuwahusisha watumiaji wa bidhaa na huduma zaidi ya 1,000.
Katika utafiti huo pia sabuni maarufu ya unga ya Foma Gold nayo imebainishwa kuwa ni bidhaa bora nchini na imetunukiwa tuzo ya SuperBrand.
Akizungumzia matokeo hayo, Ofisa Mtendaji wa Taasisi ya The Centre for Brand Analysis, Stephen Cheliotis, alisema: “Inafurahisha kuona chapa nyingi za Tanzania zinaendelea kushikilia rekodi ya ubora na kuendelea kupata tuzo za SuperBrand mwaka hadi mwaka.
“Mwaka huu chapa nyingi zimeweza kuendelea kushikilia rekodi ya kuingia kwenye chapa bora 20 zinazoongozwa kwenye masoko na mwaka huu chapa za bidhaa kwenye kundi la usafi na afya za Whitedent na Foma Gold zimefanya vizuri na zinakubaliwa na wengi kwenye masoko.”
Ofisa Mtendaji huyo alisema matokeo hayo yalizingatia maoni ya wataalamu wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ukihusisha pia makampuni ya hapa nchini yanayotumia nembo na chapa za biashara za kimataifa kama vile TOYOTA na Pepsi ambapo chapa 10 zimeingia kwenye chapa 20 bora.
Aisha alisema utafiti huo ulifanyika katika mgawanyo wa makundi ya taasisi za fedha, vyakula na vinywaji, magari na utoaji wa huduma kwa jamii.