32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

MTOTO ANAYEKULA MAFUTA KUTIBIWA MUHIMBILI

Na Veronica Romwald- Dar es Salaam

MTOTO Shukuru Kisonga aliyeteseka miaka 16, akiishi kwa kula mafuta chupa moja, maziwa lita mbili na robo tatu ya sukari, hatimaye atapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa MNH, Aminiel Aligaesha, alisema tayari madaktari wamechukua kipimo cha damu kuchunguza tatizo linalomsumbua.

“Tulipokea oda kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, tumtafute mtoto huyu ili atibiwe, wamefika jana (juzi) na tutamwangalia kwa ukaribu ili tujue tatizo linalomsumbua na tumtibu,” alisema Aligaesha.

Mwanabibi Mtete ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo, alisema ana imani mtoto wake atapata matibabu na kupona.

“Mimi ni mjane, mwanangu ameteseka kwa muda mrefu, sikuwa na fedha za kutosha kulipia matibabu kwani ni ghali, kila alipokosa vitu hivyo ili ale aliumia.

“Mwili wake ulikuwa unakatakata mfano wa gari lililoishiwa mafuta, ilibidi nimsaidie kwa kumkandakanda kwa mikono yangu, hali hiyo ikimtokea shuleni wenzake humbeba na kumrudisha nyumbani,” alisema.

Alisema Shukuru kwa sasa yupo kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mgomba iliyopo Tunduru mkoani Ruvuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles