25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAAFA Z’BAR YAMSONONESHA DK. SHEIN

Na Mwandishi Wetu

-ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amehuzunishwa kwa kiasi kikubwa na maafa yaliyotokea Unguja na Pemba kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kutokana na hali hiyo amewaahidi wananchi kuwa Serikali yao itahakikisha inawapa misaada inayohitajika pamoja na kuzifanyia kazi athari zilizotokea ikiwamo uharibifu wa miundombinu ya barabara.

Kauli hiyo aliitoa jana katika ziara yake aliyoifanya katika maeneo mbalimbali ya Unguja yaliyoathirika na mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha ambazo zimepelekea baadhi ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba zao kubomoka, kuharibika kwa miundombinu ya barabara, madaraja pamoja na kuharibika kwa mazao.

Miongoni  mwa maeneo aliyoyatembelea katika ziara yake hiyo ni eneo linalotuama maji Mwanakwereke, kuangalia mafanikio ya ujenzi wa mtaro mkubwa wa kupitishia maji kupitia Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) huko Karakana, Bumbwisudi kwa Goa, Mwera Gudini, Fuoni Kibonde Mzungu,  Daraja la Mwanakwerekwe Nyumba Mbili ambapo katika Mkoa huo wa Mjini Magharibi ambapo nyumba 1,130 zimeathirika na mvua hizo.

Katika ziara yake hiyo ambayo viongozi mbali mbali walishiriki, Dk. Shein pia, alipewa taarifa mbali mbali kutokana na athari za mvua hizo za masika kutoka kwa viongozi husika ambao pia, walieleza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa sambamba na azma ya Serikali katika kukabiliana na maafa kama hayo katika maeneo yaliyoathirika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles