25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

WENYE VYETI FEKI KUFUTIWA HADI PHD ZAO

RAMADHANI LIBENANGA Na NORA DAMIAN (Moro, Dar)

SERIKALI imesema watumishi wa umma wenye shahada ya kwanza hadi ya tatu ambao watabainika kughushi vyeti vya kidato nne na sita watafutiwa taaluma zao.

Wakizungumza na MTANZANIA jana, Naibu Makatibu Wakuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila na Dk. Avemaria Semakafu, walisema kosa lolote la kitaaluma linapobainika kwa mujibu wa sheria litasababisha kufutwa   taaluma ya muhusika.

Makatibu hao walikuwa wakizungumza baada ya kufungua mkutano wa baraza la 24 la wafanyakazi wa wizara hiyo   mkoani hapa.

 "Hata kama ukiwa na elimu ya juu kiasi gani lakini ikibainika kuna ngazi moja umeghushi basi kwa mujibu wa kanuni taaluma yako itafutwa mara moja," alisema Profesa Msanjila.

Alisema   zipo mamlaka maalumu zikijiridhisha kama muhusika ana vyeti feki basi taaluma yake itafutwa bila pingamizi lolote.

Naye Dk. Semakafu alisema lengo la uhakiki wa vyeti feki ni kuwa na watumishi wenye sifa na weledi kwa mujibu wa elimu stahiki.

Alisema   ukaguzi wa vyeti ni mkakati wa siku nyingi lengo likiwa ni kuboresha elimu nchini.

"Lengo ni kila mtu akae kwenye nafasi na viwango stahiki," alisema Dk. Semakafu.

Awali akifungua mkutano huo, Profesa Msanjila aliwataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kuwa wabunifu kutokana na mabadiliko.

Alisema serikali imejipanga kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu na   imeweka vipaumbele vya msingi   kuinua ubora wa elimu katika nyanja zote. 

"Serikali imejipanga kuwa na elimu yenye ubora katika viwango vya ndani na nje ya nchi  kwa kusambaza vifaa  vya maabara,  hivyo acheni kufanya kazi kwa mazoea. Mnatakiwa kujituma kwa weledi mkubwa na kuangalia matokeo ya kazi,” alisema.

Wakati huo huo, Serikali imesema watumishi ambao wamekata rufaa baada ya kubainika kuwa na vyeti feki hawaruhusiwi kuendelea na kazi hadi rufaa zao zitakaposikilizwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles