30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAKARABATI VYUO 10 VYA UALIMU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Simon Msanjila

 

 

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

SERIKALI imekarabati vyuo 10 vya ualimu kati ya 35 kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia walimu.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Simon Msanjila, alipofungua mafunzo ya mradi wa kuimarisha elimu ya ualimu.

“Hawa wanabeba jukumu kubwa la kuwasaidia watoto wetu, hivyo ni lazima Serikali iwaangalie na ndiyo maana tukakarabati vyuo 10 na hivi vingine vitaingia katika bajeti inayofuata,’’ alisema.

Pia alisema wameamua kutoa mafunzo hayo ili wakuu wa vyuo wajue namna bora ya kufanya ununuzi katika vitu mbalimbali.

 “Katika ununuzi kuna utaratibu wa kufuata, kila kinachonunuliwa lazima thamani ya fedha ionekane, sio unakurupuka tu kujinunulia, lazima uangalie na bei ya soko ikoje.

 “Mradi huu utakuwa ni wa miaka mitatu na umejikita katika kutekeleza na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa walimu pamoja na kujua mbinu mbalimbali za kufundishia na kuboresha miundombinu katika vyuo vyetu,’’ alisema.

Pia alisema Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika elimu, lengo likiwa ni kuhakikisha elimu inakuwa njia ya kumkomboa Mtanzania.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Bajeti wa wizara hiyo, Gerald Mweri, alisema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia walimu.

Mweri ambaye pia ni msimamizi wa mradi huo, alisema umegharimu jumla ya Sh milioni 83 na changamoto kubwa wanayokutana nayo ni walimu wakuu wa vyuo kutojua namna ya kufanya ununuzi.

“Ununuzi ni tatizo, ndiyo maana tupo hapa kuwapa ujuzi na namna bora ya kufanya ununuzi katika vitu mbalimbali,’’ alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles