24.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

WANAWAKE WAKUMBUSHWA WAJIBU WAO

Na RAMADHAN HASSAN-CHAMWINO


WANAWAKE wametakiwa kuwafundisha watoto wao mbinu za kuepuka ngono wakiwa na umri mdogo.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na mwezeshaji Josephine Pamila, wakati wa mafunzo kwa waelimisha rika wa Kata za Mlowa Barabarani, Mlowa Bwawani na Mpwayungu yaliyofanyika Mpunguzi, Wilaya ya Chamwino mkoani hapa.

Mradi huo unatekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la Wowap ambalo hujishughulisha na ushawishi na utetezi kwa wanawake na watoto.

“Wazazi na walezi wana wajibu wa kuwafundisha watoto wao mbinu za kujiepusha na ngono katika umri mdogo ili waweze kuepuka mimba za utotoni.

“Sababu kubwa za mimba za utotoni ni watoto wengi wa kike kukosa elimu inayohusiana na madhara ya mimba hizo, kwani baadhi yao hawaelewi mabadiliko wakati wa kupevuka na kushindwa kuhimili mihemko.

“Kwa upande mwingine, wazazi wamekuwa wakilazimisha watoto wao kuolewa na wengine kutoona umuhimu wa elimu kwa watoto wao wa kike na wakati mwingine ni tamaa za wazazi kupata mali.

“Kwa hiyo, lengo la mafunzo haya ya kuwaelimisha waelimisha rika ni kuwafanya waelewe kwa undani suala la ndoa na mimba za utotoni na madhara yake,” alisema Pamila.

Alitaja madhara ya mimba za utotoni kuwa ni pamoja na ongezeko la vifo vya uzazi na kukatiza masomo na kutokamilisha malengo katika maisha.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Magreth Ndosi, alisema bado kuna changamoto kubwa kwa wazazi kuwaoza watoto wakiwa na umri mdogo hasa maeneo ya vijijini.

“Utakuta mzazi anaoza mtoto wake kwa mahari ya shilingi 300,000 na anafanya hivyo kwa sababu anaona fedha zina thamani kuliko maisha ya mtoto wake ambaye anahitaji kuendelea na elimu na kutengeneza maisha yake ya baadaye,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles