26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

RC ATAKA MIFUGO IONDOLEWE MAPORI YA AKIBA

Na Renatha Kipaka


MKUU wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Mstaafu, Salim Kijuu aliagiza wafugaji wanaotumia mapori ya akiba kwa ajili ya malisho ya mifugo wawe wameondoka katika mapori hayo vinginevyo nguvu ya sheria itachukuliwa dhidi yao.

Alitoa agizo hilo jana  alipozungumza na waandishi wa habari.

RC alisema  kutokana na uharibifu mkubwa ambao umekuwa ukifanyika katika mapori hayo ametoa siku tatu kwa wafugaji wanaotumia mapori kuondoka.

 Alisema   hivi karibuni alitembelea  mapori ya Biharamulo, Nyantakara, Burigi  na Ruiga na kujionea hali halisi ya uharibifu wa hifadhi hizo.

RC alisema uharibifu huo ulitokana na shughuli za  binadamu   na uchungaji wa mifugo.

Alisema uharibifu unaofanyika katika hifadhi hizo ni ukataji wa miti ovyo, shughuli za kilimo ndani ya misitu na kwenye vyanzo vya maji.

Jenerali Kijuu alisema  makundi ya wanyamapori yanatishiwa kutoweka  pamoja na    uoto wa asili.

 Alisema kwa sasa wanyamapori wamechanganyikana na makundi ya n'gombe jambo ambalo linasababisha    wanyama pori   kuhama kutoka katika makazi yao ya asili na kuvamia makazi ya wananchi.

 “Niseme tu nguvu hii siyo nguvu ya soda.  Yeyote atakayekaidi agizo hili la kuondoka ndani ya siku tatu atataifishiwa mifugo yake,”alisema.

Alisema  kutokana na mvua inayoenderea kunyesha, wananchi hawana budi watumie frusa hiyo kulima  mazao ya chakula ili kuwa na akiba ya chakula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles