32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

CCM, CHADEMA WAFUNGUA MILANGO UCHAGUZI EALA

Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), vimefungua rasmi pazia la kuwania nafasi za wajumbe watakaoiwakilisha nchi katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Taarifa kwa vyombo vya habari zilizotolewa kwa nyakati tofauti na vyama hivyo jana, zimetanabaisha kwamba mchakato wa kuchukuwa fomu tayari kwa mnyukano huo umefuguliwa rasmi. Chadema wameanza kutoa fomu hizo jana huku CCM wakitarajia kuanza leo.

Kwa mujibu wa taarifa ya CCM iliyotolewa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, wanachama wa chama hicho wanaotaka kuomba ridhaa na dhamana ya ujumbe wa Bunge la EALA wametakiwa kuchukuwa fomu leo na kurejesha Machi 23.

“Vituo vya kuchukulia fomu ni Makao Makuu ya CCM Dodoma, Ofisi Kuu ya Makao Makuu Zanzibar na Ofisi Ndogo ya Makao Makuu Dar es Salaam katika Idara ya Organizesheni.

“Aidha inasisitizwa na katika muktadha na uhalisia wa mageuzi makubwa ya chama chetu ambayo yanalenga kutupatia aina ya viongozi waadilifu, waaminifu, wachapakazi, wawajibikaji, wanaochukia rushwa, wanaoweka masilahi ya chama na nchi mbele, kwamba waomba ridhaa na dhamana ambao wataonyesha kwa mwenendo na vitendo kukiuka Katiba ya CCM, kanuni za uchaguzi CCM na kanuni za uongozi na maadili za CCM, uongozi  na vikao vya chama havitaona ajizi kuchukua hatua kali ikiwemo kuwaondolea sifa ya uteuzi,” imefafanua taarifa hiyo.  

Kwa upande wa Chadema, uchukuaji wa fomu utafikia ukomo Machi 21 na Machi 22 uteuzi utafanyika.

Chadema kimewataka wanachama wake wote ambao wana sifa na vigezo vya kuwania nafasi hiyo kuchukua fomu katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, ofisi za kanda za kanda 10 ambazo zipo Tanzania Bara na Zanzibar na ofisi za mikoa na majimbo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles