26.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

BOSSOU AMEIZOEA TANZANIA AMEKUWA MSWAHILI

Na MARTIN MAZUGWA


‘IF you go to Rome do what’s Romans do’ ni msemo wa Kiingereza wenye maana kuwa ukienda Roma fanya kile wanachokifanya Waroma, ni msemo wenye maana kubwa iwapo utatafsiriwa kwa ufasaha.

Si kwamba unatakiwa kufuata kila kitu kiwe kizuri au kibaya unapaswa kufuata mazuri pekee ambayo yatakujenga vyema katika misingi inayopendeza na ambayo haitokufanya utofautiane na wenyeji wako, lakini pia usivunje sheria za nchi huku mabaya ukiyafanya kama funzo kwako.

Klabu ya Yanga ina jumla ya wachezaji saba wa kigeni kutoka katika mataifa manne ikiwamo Zambia, Rwanda, Togo pamoja na Zimbabwe, imefanya usajili huu ili kuimarisha kikosi chake katika michuano mbalimbali kama vile Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Kombe la FA pamoja na Ligi ya mabingwa barani Afrika ambayo imeingia raundi ya pili mara baada ya kuitoa Ngaya Club ya visiwa vya Comoro.

Moja kati ya wachezaji wa kigeni waliokuwa wakiheshimika sana na klabu zao ni mlinzi wa kati wa klabu ya Yanga, Vicent Bossou raia Togo, aliyekuwa na heshima sana kwa vijana wa Jangwani, huku akiwa na nidhamu ya hali ya juu uwanjani na kuwa kipenzi cha mashabiki waliokuwa wakikubali uwezo wake.

Lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda, namwona Bossou mpya ambaye amekuwa na kiburi na jeuri hadi kwa vyombo vya habari hadi kwa mwajiri wake ambaye amemtoka Togo kwa kazi, naanza  kuiona tabia ya Kiswahili ndani yake jambo ambalo ni hatari kwa kibarua chake katika timu ya Yanga pamoja na maendeleo ya soka lake.

Ule msemo wa wahenga wa ukitaka kuishi Roma,  hatimaye umemvaa kisawa sawa Bossou na kumpendeza siku hizi hana hofu tena, huku akisahau kuwa klabu ya Yanga ni kubwa kuliko yeye na ina ushawishi mkubwa kutokana na wingi wa mashabiki wake ambao wamekuwa wakiiheshimu nembo ya klabu yao.

Sijui kama anajua anachofanya kuwa anakosea,  lakini huwa sipati shida katika hili kujua kwani si kwa raia huyu wa Togo pekee bali wachezaji wengi wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali wamekuwa wakibadilika sana pindi wanapoanza kuiga tabia za wachezaji wa Kiswahili.

Bossou anatakiwa ajue hii ni Tanzania, mashabiki wake wapo kwa ajili ya kushangilia na kuzomea, iwapo utateleza na kuanguka usitegemee kuwa utainuliwa na kukung’utwa vumbi kwa mchango wako ulioutoa kwa timu.

Kitendo cha kuandika katika ukurasa wake wa kijamii na kuituhumu klabu kubwa kama Yanga kwamba haijamlipa mshahara ni tusi na kuipaka matope timu hiyo kubwa yenye mashabiki wengi nchini Tanzania.

Wakati unaendelea kuposti kuwa hujalipwa uongozi wa klabu wa Yanga unakanusha kuwa unaidai klabu mshahara wa mwezi wa pili pekee, kwa hili Bossou umefeli nenda ukakae na waajiri wako uzungumze jambo la kukaa na kutoa shutuma wakati huna uhakika unashusha heshima yako kwa wapenzi wa klabu ya Jangwani ambao walikuamini na kukuthamini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles