32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Milioni 30 zampeleka Mgezeke Simba

mgezeke
Joram Nason Mgeveke akisaini mkataba wa kuichezea Simba

NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

MLEZI wa timu ya Lipuli ya Iringa, Cyprian Kwihyava, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Iringa (IRFA) juzi walikamilisha taratibu za mwisho na uongozi wa Simba, kuhusiana na usajili wa mchezaji wao Joram Mgezeke, huku Simba zikiwatoka Sh milioni 30 kumpata.

Mgezeke ambaye ni beki wa kati wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ameshasaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Simba, kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na hivi sasa yupo nchini Botswana kwenye kambi ya Stars.

Habari toka ndani ya Simba zinadai, juzi aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alimalizana na mlezi huyo wa Lipuli kwa ada ya uhamisho ya mchezaji huyo.

“Hans Poppe kashamalizana nao kuhusiana na kiasi cha fedha walichokuwa wametuambia, tuliingia naye mkataba wa miaka mitatu wiki iliyopita hivyo kwa sasa tunaendelea na vita vingine vya usajili,” kilieleza chanzo hicho.

Naye Katibu Mkuu wa Lipuli aliyemuibua Mgezeke kutoka mchangani, Willy Chikweo alisema hafahamu lolote kuhusiana na suala hilo kwani wamemuachia mlezi wa timu hiyo kushughulikia, huku akidai Hans Poppe ndio sababu ya kumuuza mchezaji huyo Simba.

“Unajua Hans Poppe ni mtu wa Iringa anaisaidia kwa hali na mali timu hii, ndio maana tuliipa kipaumbele Simba kumyakua na hata Simba yenyewe itatupa baadhi ya wachezaji wake kwa mkopo katika msimu ujao wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL),” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles