24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Maswa washitakiana kwa Silaa

NA SAMWEL MWANGA

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wamewalalamikia viongozi wao wakidai wanaendekeza makundi.

Kwa mujibu wa wanachama hao, hali hiyo ilichangia kupoteza viti vya ubunge katika majimbo ya Maswa Mashariki na Maswa Magharibi katika uchaguzi mkuu uliopita.

Hayo yamebainishwa juzi mbele ya

Jerry Silaa
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Jerry Silaa

na viongozi wa matawi na kata wa chama hicho wilayani humo katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.

Baadhi ya wanachama hao walisema makundi hayo ndani ya chama hicho hasa wakati wa kura za maoni yameendelea hadi sasa.

Wamesema hali hiyo imekiweka chama hicho njia panda na wasiwasi wa kushinda uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani.

Mwananchi mmoja, Boniphace Budodi aliwatupia lawama viongozi wa chama hicho wilayani humo kwa kutokuwa na mshikamano.

Budodi alisema viongozi wamekuwa vinara wa kuyaendeleza makundi kutokana na ubinafsi na uroho wa madaraka hali ambayo aliisema kuwa ni sawa na kansa inayokitafuna chama.

“Mheshimiwa MNEC, hapa tuseme ukweli upungufu mkubwa ndani ya CCM Maswa ni kushindwa kuvunja makundi kwani kila kiongozi hapo hapo yupo mezani ana kundi lake na hao ndiyo wanakididimiza chama. Hata ukiangalia kamati ya siasa ya wilaya ni vipande vipande hivyo tatizo ni viongozi wetu hao uliokaa nao,”alisema Budodi.

Wanachama hao walisema bila upungufu huo kufanyiwa kazi ni ndoto kwa CCM kufanya vizuri katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na ubunge ikizingatiwa viongozi hao wamekuwa wakithubutu hata kuwatolea lugha ya matusi wazee ndani ya chama hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles