25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

WADAU WAPONGEZA WASAIDIZI WA SHERIA

Na JUSTIN DAMIAN 

BAADHI ya wadau wanaofanya kazi sekta ya sheria, wameelezea kuridhishwa  na hatua ya Bunge kupitisha Sheria ya Huduma za Msaada wa Kisheria

Wadau hao, wamesema hatua hiyo itasaidia upatikanaji wa haki kwa wanyonge, hasa wanawake na watoto wanaoishi pembezoni mwa Tanzania.

Akizungumza wakati akikabidhi kompyuta 170 kwa wasaidizi wa kisheria zilizotolewa na Mfuko wa Sheria(LSF), Balozi wa Denmark hapa nchini, Einar Jensen alisema ana imani sheria ya msaada wa kisheria, itapanua wigo kwa wananchi maskini kupata msaada wa kisheria.

Aliwataja wasaidizi wa kisheria kama nguzo muhimu ya kusaidia watu wasiokuwa na uwezo wa kulipia huduma za kisheria zinatolewa na wanasheria na mawakili.

“Wakitambuliwa na sheria ni hatua nzuri inayopaswa kupongezwa.

“Baada ya sheria hii kupitishwa bungeni, inatoa uwanja mpana kwa wananchi wa kawaida kupata haki zao, kupitia huduma zinazotolewa na wasaidizi wa kisheria,” alisema balozi.

Aliongeza kuwa kompyuta zilizotolewa kwa wasaidizi wa kisheria zitasaidia kuongeza ufanisi katika kazi zao ikiwa ni pamoja na kurahisha upatikanaji wa taarifa na kuwawezesha wasaidizi kuwasiliana na wenzao katika kukuza utunzaji wa kumbukumbu za wananchi wenye matatizo mbalimbali ya kisheria.

 Balozi Jensen, alisema wasaidizi wa kisheria nchini kila mwaka huwafikia wananchi wasipoungua 40,000 sawa na asilimia 54 wenye kero mbalimbali na 70 ya matatizo yao yalipatiwa ufumbuzi wa kudumu.

 Kwa upande wake, mjumbe bodi ya LSF, Dk. Benson Bana alielezea kufurahishwa kwake na hatua sheria mpya ya wasaidizi wa kisheria, na kusema kuwa itaongeza hari kwa wasaidizi wa sheria katika kutatua kero za watanzania.

Alisema sasa wigo wa upatikanaji wa haki za wananchi za mirathi, ardhi na ndoa na kupunguza ukubwa wa matatizo kwa wanannchi hasa wa maeneo ya vijijini.

Afisa Mradi wa LSF, Fortunata Kitokesya alisema kompyuta mpakato 170, zenye thamani ya Sh milioni 150 zitarahisha utendaji wao wa kila siku.

Ofisa  Mtendaji Mkuu wa mfuko huo, Kees Groenendijk alisema upatikanaji wa kompyuta hizo ni hatua muhimu kwa wasaidizi wa kisheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles