27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

SERIKALI YAWATEMBELEA WATANZANIA WANAOSHIKILIWA MALAWI

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi jana aliwatambelea Watanzania wanane wanaoshikiliwa katika Gereza Kuu la Mzuzu nchini Malawi kwa tuhuma za kuingia kinyume cha sheria katika mgodi wa urani wa Kayerekera.

Katika ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu  aliandamana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma (RAS), Hassan Bendeyeko na maofisa wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi.

Taarifa iliyotolea kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana,ilisema Serikali imewasihi watu hao kuwa wavumilivu wakati suala hilo likishughulikiwa.

Balozi Mwinyi, alisema mazungumzo yamepita ngazi mbalimbali kati ya Tanzania na Malawi, yanaendelea na kuna matumaini makubwa ufumbuzi kupatikana hivi karibuni.

Alisema yeye na wenzake, wamekwenda Lilongwe kushiriki kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi,lakini wameamua kusafari  takriban kilomita 400 kutoka Lilongwe  hadi Mzuzu kuwaona na kuwafikishia ujumbe kuwa Serikali inafanya jitihada za kuwatoa.

"Napenda kuwafahamisha kuwa jitihada katika ngazi mbalimbali kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo lenu zinaendelea,hata Rais Dk.John Magufuli alipokutana na Rais wa Malawi, Profesa Peter Mutharika pembezoni mwa mkutano wa wakuu wa nchi wa Umoja wa Afrika nchini Ethiopia, jambo lenu lilikuwa moja ya masuala  waliyoyajadili,”alisema Balozi Mwinyi.

Alisema alifarijika kuwakuta wote wapo salama na wenye afya nzuri.

Watanzania wanane, walikamatwa mwishoni mwa Desemba,mwaka jana hadi sasa wanashikiliwa gereza kuu la Mzuzu, kati yao wawili ni wanawake  wamejitambulisha ni wakulima na wachimbaji wadogo wa madini wanatoka Mkoa wa Ruvuma na walikwenda Malawi chini ya Taasisi ya CARiTAS kujifunza athari za migodi ya urani katika jamii.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles