26.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Ugonjwa wa kisukari waahirisha kesi

Na Maneno Selanyika, Dar es Salaam

KESI ya kumtesa mfanyakazi wa ndani inayomkabili Wakili wa kujitegemea, Yasinta Rwechungura (44), inaendelea leo baada ya kuahirishwa jana kutokana na Wakili wa Utetezi kusumbuliwa na kisukari. Akitoa sababu ya kuahirishwa kesi mahakamani hapo, Wakili wa utetezi, Benitho Mandele, alisema anasumbuliwa na kisukari hivyo asingeweza kusikiliza kesi hiyo. “Mheshimiwa mimi nipo tayari kumwakilisha mtuhumiwa ila ugonjwa huu unatokea wakati wowote na kwa sasa sijisikii vizuri hivyo ninaomba shauri lililopo mbele yako kwa ajili ya ushahidi uliahirishe kwa tarehe ya karibu,”alidai Wakili Mandele. Wakili upande wa Jamhuri, Masini Mussa, alionekana kutoridhishwa na maelezo ya wakili wa utetezi kwa kuwa shauri hilo ni la muda mrefu hivyo aliiomba mahakama iliangalie hilo. Mussa alidai kuwa baada ya tukio la kuteswa kwa msichana, Merina, mlalamikaji alipelekwa sehemu isiyojulikana ili haki isitendeke. Alidai wasamaria wema walimtafuta na kumrudisha na leo hii yupo mbele ya mahakama tayari kwa kutoa ushahidi. “Mheshimiwa nimesikiliza hoja za wakili wa utetezi lakini atambue kuwa kuna jitihada kubwa zimefanyika kumleta mahakamani mlalamikaji kwa sababu baada ya tukio alisafirishwa hadi mkoani Kagera. “Mheshimiwa Merina alipofichwa sehemu isiyojulikana walijitolea wasamaria wema kwenda hadi Bukoba kumchukua huyu mtoto kwa kuwa waliompeleka huko walikuwa na nia ovu na walitaka haki isitendeke. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Amalia Mushi, alisema kwamba ameridhishwa na hoja za pande zote mbili hivyo alitoa uamuzi kwamba kesi hiyo iendelee leo saa 3:00 asubuhi. Wakili wa Kujitegemea, Yasinta Rewchungura anadaiwa kuwa Juni 11 mwaka jana eneo la Boko Njia Panda, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, alimpiga mfanyakazi wake wa ndani, Merina Matayo (15) kwa waya wa kompyuta na jagi la juisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles