27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MABADILIKO SHERIA ZA UVUVI YAJA

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba

Na ASHA BANI, Bagamoyo

SERIKALI inatarajia kuwasilisha Bungeni mabadiliko ya sheria na kanuni kwenye sekta ya mifugo kudhibiti wavuvi haramu na kuongeza pato la taifa kupitia sekta hiyo.

Imeelezwa pia kuwa ni asilimia 40 tu  ya ukanda wa bahari ndiyo   haijaharibiwa huku asilimia 60 ikiwa imeharibiwa kutokana na shughuli za binadamu hasa uvuvi haramu.

Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba wakati wa uzinduzi wa kifaa kitakachotumika kuvutia samaki katika eneo moja na kuvuliwa kwa urahisi.

Kifaa hicho pia kinaweza kuitwa chambo kutokana na uwezo wake wa kukusanya samaki katika eneo moja la bahari na   kuvuliwa bila kutumia njia haramu kama vile baruti na mabomu mengine.

Akizungumzia   mabadiliko ya sheria, Dk. Tizeba alisema mabadiliko ya kwanza ya sheria yatambana  mvuvi kutoka nje ya nchi ambaye atatakiwa kulipa mrabaha kulingana na samaki aliovua.

Mabadiliko ya pili ni katika kuhakikisha mabaharia wazalendo wanashirikishwa kwenye vyombo vya uvuvi  vijana nao waweze kupata ajira.

Mabadiliko ya tatu ni kuhakikisha   samaki wanaovuliwa nchini wanakuwa na vibali hata kama wanasafirishwa nje ya nchi.

Alisema  kama wakikamatwa katika nchi nyingine huku wakiwa hawajalipia kibali chochote, watakuwa ni mali ya Tanzania na wahusika watanyang’anywa.

Mabadiliko ya nne ni makubaliano ya ukaguzi wa mara kwa mara, alisema.

Dk.Tizeba alisema   hiyo itasaidia kudhibiti uvuaji wa samaki holela na kusaidia kuongeza mapato yanayotokana na uvuvi

‘’Utekelezaji wake katika hili ni kuhakikisha wavuvi wote wanavua kwa kufuata sheria na kanuni hizo na  tayari baadhi zimeshatangazwa kwenye gazeti la serikali,’’alisema Dk.Tizeba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles